Tuesday, September 18, 2012

Dr Mwanjoka asimikwa

Baada ya Uchaguzi wa August 9,pale UDOM wa kanisa la TAG,jimbo la Nyanda za Juu Mbeya lilipata askofu Mpya Dr Donald Mwanjoka ambaye leo amesimikwa na hivyo kutangazwa rasmi kuwa ndiye askofu wa Nyanda za juu Mbeya.
Ibada hiyo ya kusimikwa iliongozwa na askofu Mkuu wa kanisa la TAG,Dr Barnabas Mtokambali.
Kabla ya kuanza tendo hilo la kuwasimika,Askofu Mtokambali aliweka wazi utaratibu wa kuwapata viongozi wa kanisa la TAG na alisema wanapatikana kwa njia ya Maombi na si kwa Kufanya kampeni,kwa ubaguzi wa kikabila ama kwa kutoa rushwa...hivyo akamalizia na kusema Dr mwanjoka ndiye Chaguo la Mungu kwa wakati huu baada ya Mungu kujibu maombi ya waamini,washirika na kanisa kwa ujumla.
Pia Dr Mtokambali alitumia nafasi hiyo kufikisha ujumbe kwa serikali...na alisema serikali yetu inatakiwa kutumia nguvu zake zote katika kulinda Amani ya Nchi yetu,Ushirikiano na Umoja wetu.
Pamoja na Dr Mwanjoka,walisimikwa pia makamu askofu wa jimbo Rev Adson Mwajunga na katibu Rev.Peter Masika.
 Sherehe hizo zilifanyika katika kanisa la ICC-Ikuti(International Christians Centre) ambalo ni kanisa linalochungwa na Askofu Dr Donald Mwanjoka.Leo tarehe 18/09/2012 kuanzia saa 3 asubuhi mpaka na kumalizika majira ya saa 10 jioni
Pamoja na hayo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya ambaye hata hivyo hakuweza kufika aliwakiliswa na DAS(katibu Tawala).

Sunday, September 2, 2012

Kwa nini Mungu akutendee wewe

Ili Mungu akutendee kuna shughuli...maana kuna kundi la watu kila siku kila saa wanapiga magoti mahali fulani wakiomba Mungu nao watendewe lile lile unaloomba wewe au zaidi ya la kwako...swali kwa nini akutendee wewe na awaache wengine.
Ni maneno yaliyosemwa na Pastor Matthew sasali alipokuwa akihubiri jumapili ya leo katika kanisa la TAG Galilaya(Katumba-Tukuyu).

Sunday, August 26, 2012

Steps to becoming the Vessel of Honour

Ili kuwa mtu wa kiMungu ambaye watu wata-admire maisha yako,lazima upite kwenye mchakato waKiMungu(God`s person thru God`s process),Na mara zote mchakato wa kiMungu si mwepesi.
Mara zote Mungu hufanya kazi kuhakikisha,tunakaa katika ile taswira ambayo ameikusudia katika maisha:hayo yalisemwa na Pastor Matthew sasali katika utangulizi wa ujumbe wake asubuhi ya leo,katika kanisa la Rehoboth International Christian Centre,jijini Mbeya wakati wa mahubiri yake,ibada ya kwanza na ya pili.
  Kifungu kilichotumika ni Yeremia 18:1-6,wakati Mungu akimsikilizisha Nabii Yeremia neno lake juu ya Taifa la Israel.
Pastor Matthew alisema,kama unataka kuwa chombo cha heshima kwa ajili ya huduma ya kiMungu,ni lazima ukubali kuchongwa na Mungu kwa namna ile ambayo Mugnu mwenyewe anataka...na hiyo ni kazi ya MUNGU mwenyewe.
Kabla ya kuanza kutaja hatua hizo alitaka kanisa lijue mambo mawili kwanza ya msingi
1.Taswira ya chombo kinavyotakiwa kuwa iko mawazoni mwa Mfinyanzi mwenyewe
Watu wengi hudhani wao ndio wanaoweza kutabiri na kufanya kile ambacho wao hutamani katika huduma zao...mwisho wa siku tunatengeneza matakwa yetu na si matakwa ya Mungu.
2.Sisi kama udongo na Mungu kama mfinyanzi ni lazima kwa unyenyekevu na adabu,tukubali kukaa mikononi mwa mfinyanzi ili mwisho wa Mchakato tuwe kile ambacho Mungu amekusudia.
Ni rahisi kukosa unyenyekevu na subira na kukimbia katikati ya mchakato,na wengi hufanya hivyo...mwisho wa siku,hatutokei kile ambacho mfinyanzi amekikusudia.
Akaendelea na kusema Mungu yeye kama mfinyanzi anayajua maisha yetu ya zamani,ya sasa na ya baadaye,hivyo wakati anafanya kazi yake na sisi tayari anakuwa ameona kile ambacho tunatakiwa kukikamilisha katika maisha yetu ya baadaye.
 Hatua za Kuwa chombo cha Heshima
1.Ni lazima mfinyanzi akusanye Udongo kutoka ardhini na kisha autenge na uchafu(ausafishe).
Ili kuwa chombo cha heshima,lazima ukubali kutakaswa na kuoshwa dhambi kwanza,maana huwezi kufika ngazi ya kuwa chombo cha Heshima huku ukiwa mwenye dhambi,la sivyo chombo kilichotengezwa bila udongo wake kuoshwa ipasavyo ni rahisi kuvunjika hata kama kinang`aa namna gani.
2.Mchakato huo wa Kuoshwa kwa udongo hukamilishwa na Maji...udongo hulowekwa ili kuuchambua na kisha kuwa laini ili kumrahisishia mfinyanzi kufanya atakavyo...maji ni Roho mtakatifu,Mtu wa Mungu lazima awe na ujuzi binafsi na roho mtakatifu maana humo ndimo karama,huduma,tabia,mienendo hulainishwa na kufanywa utayari kwa mfinyanzi kumtumia mtu.
3.Ukitazama picha ya Mfinyanzi,utadhani anazombana na udongo katika hatua hii ila kufanya chombo,na hii ndio hatua ambayo chombo huumbika.
Si hatua rahisi na laini,watu wengi hukimbia hatua hii...hapa ni wakati unafinyangwa,ni wakati wamaumivu,kukataliwa,kukosa chakula ama mavazi,kuachwa na marafiki...nyakati ngumu hata kutengwa ndani ya kanisa...si hatua rahisi,maana Mungu anashughulika mna maisha yako ili kufikia kusudi lake,anashughulika na tabia yako ili kukufanya ufae..wengi hukimbia hatua hii ya mchakato wa kiMungu...maana huona ni kama Mungu amemwacha na kama hujagundua kuwa uko kwenye mchakato wa kiMungu,huwa tunatumia muda mwingi kufunga na kuomba na kukemea ili hali hii ipite kando...kumbe Mungu hutucheka na kusema"huyu ni yeye mwenyewe aliomba kufinyangwa ili afae...mbona anataka kukimbia tena..."mara zote yeye anatuwazia yaliyo mema.
Kuna nyakati tunapitia kwenye nidhamu na kuona kama tunaonewa...kumbe Mungu anatuwazia yaliyo mema kwa maisha yetu ya utumisha wa baadaye.
Tukitoka kwenye hatua hizo...kila mtu hutamani huduma yetu,maisha yetu,baraka zetu,mafanikio yetu....lakini tukumbuke ili tuwe mtu wa kimungu kama alivyotukusudia ni lazima tupite kwenye mchakato wa kiMungu.

Akamaliza na kusema tunatamani maisha ya Yusufu,Ayubu,Musa,Daudi na wengine wengi kwenye biblia...siri kubwa ni lazima tuwe na unyenyekevu na kukubali kubaki kwenye mikono ya mfinyanzi hata nyakati za kufinyangwa kwetu.

Thursday, August 23, 2012

Dr Mtokambali askofu tena TAG

Ilikuwa na Nderemo na vifijo katika ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma,baada ya msimamizi wa Uchaguzi mwenyekiti wa wameshinari Africa Mashariki Rev.Gregory Beggs,kutangaza kuwa Dr Barnabas Wenston Mtokambali,ameshinda uchaguzi kwa Kura zaidi ya 1900 sawa na asilimia 93 ya wapiga kura wote.
Haikuwa rahisi kuamini hilo kwa Askofu Mtokambali,hivyo kumfanya atokwe na Machozi na kisha kuanza kuwashukuru Wajumbe wa mkutano huo na kutoa Ahadi ya kukubali uteuzi huo na kuwa yuko tayari kulitumikia shauri la Mungu kwa kipindi kingine tena cha miaka minne.
 Kabla ya Uchaguzi huo,Askofu mtokambali alitangulia kusoma ripoti ya utendaji kazi kwa kipindi chake cha kwanza cha miaka minne iliyopita,ambayo ilisheheni mambo makubwa ambayo yeye na kamati yake wamefanikiwa kuyatekeleza na kuyaanzisha,chini ya sera maarufu ijulikanayo kama MIAKA KUMI YA MAVUNO,ripoti hiyo ilionyesha namna gani gani kanisa lilivyoongezeka maradufu kimapato,kimaendeleo,kihuduma,kiidadi,watumishi na hata kimahusiano na serikali na hata kimtandao nje ya nchi.Ripoti ambayo ilichukua takribani saa moja na nusu kusomwa kwa wajumbe na kisha kushangiliwa kwa nguvu na maombi mengi ya shukrani kwa kile Bwana alichokuwa anakifanya na kanisa la TAG.
 Na punde tu baada ya kumaliza ripoti yake,Askofu atokambali alitumia dakika takribani kukemea vikali kampeni vilizokuwa zikiendelea chini kwa chini kuhusu uchaguzi huo,na kusema si sera wala mlengo wa kanisa hilo kufanya kampeni katika mchakato wake wa uchaguzi nyanja zote,na kama kanisa limefika huko liko hatarini kuachwa na Mungu.
Maneno hayo aliyasema baada ya kuwa na vuguvugu la kampeni za kikabila,kuchafuana,kielimu na hata kifedha zilizojipenyeza katika harakati za kuelekea mkutano huo wa Uchaguzi.
Dr Mtokambali alifanikiwa kuchaguliwa tena kuwa askofu mkuu wa kanisa hilo kwa miaka minne mingine kwa Mujibu wa katiba ya kanisa la TAG.
Hata hivyo,Dr magnus Mhiche aliyekuwa makamu askofu Mkuu naye alifanukiwa kurudishwa tena katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minne mingine,na kisha uchaguzi wa ngazi ya kitaifa ulikamilika baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa kanisa hilo Rev.Ron Swai maarufu kama "Chalii"kurudishwa tena katika nafasi hiyo vile vile kwa miaka minne mingine.
 Mkutano huo wa Uchaguzi kwa mijibu wa katiba ya TAG hufanyika kila baada ya miaka minne,na kamati hii iliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2008 na kuja na sera ya MIAKA KUMI YA MAVUNO ambayo imeleta dira ya maendeleo ya kanisa hilo kwa kiasi kikubwa.
Dr Barnabas W.Mtokambali,alizaliwa miaka takribani 50 iliyopita,wilayani Chunya,wazazi wake wakiwa ni wahamiaji kutoka maeneo ya ziwa Nyasa(Manda),alianza safari yake ya masomo Mkoani Kigoma(form 1&2)kisha kuhamia Sekondari ya Forest(Mkoani Morogoro) na kisha Alipata Elimu ya Juu(BA)East African School of Thelogy nchini Kenya na baadaye M.Div,M Th na kisha D.Min vyuo mbali mbali nchini Marekani kati ya miaka ya 1992 na 2005.
Alianza huduma miaka ya 1988 mjini morogoro kanisa na Bethel Revival Temple ambalo analichunga Mpka sasa kutoka utupu mpaka takribani washirika 2000 hivi sasa.
Amemuoa Mrembo GLADMERRY maarufu kwa jina la MAUA na amebarikiwa watoto watatu,JOYLINE(chuo kikuu)GLADYLINE(High school) na wa kiume Pekee OCEANNIC(primary school).
Dr Mtokambali ana historia ndefu kwa kanisa hili na katika uongozi wa kanisa hili tangu mwaka 1992 mpaka sasa amewahi kuwa Katibu wa sehemu ya Morogoro,makamu askofu wa jimbo la Mashariki,Askofu nwa jimbo la Morogoro,makamu askofu Mkuu na sasa ni askofu Mkuu.
Ni mhadhiri wa vyuo vikuu duniani(global University),Mwalimu wa Neno la Mungu,Mbeba maono ya vyuo vya kupanda makanisa na mtandao wa ujenzi wa makanisa Africa,Mchungaji wa kanisa na mahali pamoja,Mume na Baba wa Familia na mambo mengine mengi.
 Huyu Ndiye Askofu wa kanisa la TAG Dr barnabas Mtokambali.

Monday, July 30, 2012

Mkristo na Ulimwengu unaobadilika

"Namshukuru Mungu kwa nafasi hii ya kipekee sana ya mimi kuhudumu ndani ya kanisa la kilutheri tangu nimeanza kumtumikia Mungu na kanisa langu la TAG...." hayo ni baadhi ya maneno yaliyosemwa na Pastor Matthew Sasali alipokuwa akijitambulisha katika kanisa la Lutheran Forest jijini Mbeya.
Pastor Matt amekuwa na juma moja la kuhudumu na kanisa la Lutheran,Usharika wa Forest tangu tarehe 23/07 hai tarehe29/07...na hii na katika maadhimisho ya wiki la sikukuu ya vijana kanisani hapo,ambayo shamrashamra zake zilianzia jumatatu hiyo kwa semina ya vijana wote hapo kanisani kisha kilele chake kilikuwa siku ya jumapili kwa Pastor Sasali kuhudumu katika idaba zote mbili za kanisa hilo na kisha katika idaba ya jioni ya kusifu na kuabudu iliyokuwa ikiongozwa na Praise and Worship Team kutoka Kanisa la Agape(Redeemed)inayojulikana mjini Mbeya kama Super Power chini ya Mwalimu na Producer Fredy Kametta.
 Kichwa cha Ujumbe wa semina hiyo ilikuwa ni Kijana mkrist na ulimwengu unaobadilika;ambapo Pastor Matthew alifundisha kuhusu Mtazamo wa Mungu juu ya Vijana,na kusema Mungu ameweka Hazina kubwa ndani ya vijana na Mungu amewaamini vijana kwa kuwa wana nguvu,Maono na wamemshinda shetani.
Pia alisema juu ya Mtazamo wa Kanisa kwa Vijana;alieleza namana ambayo kanisa la leo halimwamini kijana na kumuona ndiye chanzo cha machafuko na vurugu ndani ya kanisa.Na aligusia kuhusu Mtazamo wa Ulimwengu na Shetani kwa vijana,ambapo kijana hutumika kama chombo cha uharibifu dhidi ya ufalme wa Mungu.
 Pastor Matt akiendelea kufundisha alionyesha kielelezo cha vijana wa biblia ambao maisha yao yamekuwa chachu kwa vijana wa kikristo kama vile Yusufu,Daniel na wenzake,Daudi n.k
Haikuwa rahisi kwa Mchungaji Matthew kuhudumu ndani ya kanisa la kilutheri,maana ni kanisa lenye taratibu tofauti na kanisa asili la Mch Matthew,lakini kwa kuwa wote hulitaja jina la Bwana na kujenga ufalme wa Mungu...haikuwa shida kwake kuhudumia Neno la Mungu kanisani hapo,na kufuata taratibu zote za kikanisa.
Na jioni katika ibada ya kusifu na kuabudu Pastor Matthew alisema imekuwa rahisi sana kwa watu kuwasifia wapenzi wao,kutumia muda mwing na wapenzi wao na kujitoa kwa kiwango cha juu kwao hivyo hupelekea kuboresha mahusiano yao na wanao wapenda...lakini imekuwa kunyume kwa Mungu,wakristo hawana maneno mengi na mazito ya kusifu na kumwabudu Mungu wala Muda wa kutosha na Mungu hivyo kufanya mahusiano yao na Mungu kudhoofu kila iitwapo leo...alihamasisha na kusema Uimbaji ni njia rahisi ya kufunua hisia za mtu,hivyo katika ibada hivyo  ya kusifu na kuabudu tuitumie kama ni nafasi adimu katika maisha yetu ya kueleza hisia zetu kwa Mungu.

Monday, July 16, 2012

What makes the Unity of The Church

Katika nyakati za leo kanisa limekuwa mhanga mkubwa wa migawanyiko,migogoro na magomvi na kumbe sababu kubwa ni kanisa lenyewe"waamini" ndio wanaosababisha hayo!
Wanasababisha hayo kwa sababu...kanisa linaacha mambo ya msingi kama vile Imani moja,roho mmoja,ubatizo mmoja...na kushikilia vitu ambavyo si msingi ambavyo huleta migawanyiko.
Hayo yalisemwa na Pastor Matthew Sasali,alipokuwa akihudumu katika kanisa la TAG sayuni huko Isanga jijini Mbeya.
Alisema yapo mambo ambayo waamini wanatakiwa kuyaishi na hayo ndio ulinzi kwa kanisa...maana kanisa hushambuliwa sana na Adui kwa kuleta vitu vidogo vidogo ambavyo kama hawatakuwa makini...migawanyiko na malumbano havitaliacha kanisa.
Akitaja vitu hivyo Pastor Matthew alisema
1.Watu wanaacha mambo ya msingi yanatotuunganisha na kuweka mkazo kwenye vitu vidogo vya kututofautisha kama vile Haiba,Uwezo,Utashi....Mungu kama baba yetu alituumba tofauti na mara zote hufurahia tofauti zetu...na yeye anapenda tuwe na umoja na sisi tufanane...unity and not uniformity.
2.Lazima waamini wachague kutia moyo na si kukosoa kila jambo.
Ni rahisi kukaa pembeni na kunyoosha kidole cha kukosoa kwa mtu anayetenda jambo,ila ni ngumu sana mtu kuwa sehemu ya kutia oyo jambo linalotendwa.
 #kwa kukosoa mtu huaribu ushirika wake na Mungu
#kwa kukosoa mtu hufunua kiburi chake
#kwa kukosoa mtu hujiweka mahali pa yeye kuhukumiwa
#kwa kukosoa mtu husababisha maumivu katika kundi la Mungu.
3.Wengi hujua kuwa usengenyaji ni dhambi na huishia hapo...Pastor matthew akaendela kufundisha na kusema,lazima waamini wachague Kukataa kusikiliza Masengenyo
Kwa kukataa kusikiliza Umbeya kunaleta ulinzi ndani ya kaisa la Mungu ambalo leo hii limekuwa likisumbuliwa sana na Umbeya na masengenyo.
4.Ni muhimu waamini wakachagua Kumtia Moyo Mchungaji ama viongozi wa kanisa.
Hii inamaanisha uwepo umoja wenye kujenga kati ya Mchungaji na viongozi wa kanisa...kwani Mungu huweka maono ya mwelekeo wa kanisa kwa mchungaji na yeye atawajibika mbele za Mungu kwa ajili ya washirika wake...

Sunday, July 8, 2012

Characteristics for Giant Christians

Imekuwa kawaida kwa wakristo wengi kutamani maisha ya "Giant" wa kwenye biblia,bila kujua siri nyuma ya umwamba wao wa kiroho...hivyo wengi wakishindwa kufika hapo,huishia kuona maisha ya hao yalikuwa kama hadithi za enzi hiyo.
Mch Matthew Sasali,ameeleza hayo leo katika ibada ya asubuhi katika kanisa la Rehoboth Internetional Christian centre,Forest Mpya jijini Mbeya,wakati akifundisha sifa za watu bora"wakuu" wa biblia na kutia shauku kwa wakristo wa leo kuambatana na sifa hizo ili wawe bora zaidi ya hao wa zamani wa biblia.
Pastor Matt alifundisha kuhusu watu tisa wakuu wa biblia na kuibua siri zilizowajenga hao,Huku akisema wakristo wa leo tunatakiwa kuwa na vigezo hivyo...
1.Imani kama ya Ibrahimu
2.Uongozi kama wa Musa
3.Ujasiri na Ushawishi kama wa Daniel
4.Bidii kama ya Paulo
5.Uaminifu kama wa Timotheo
6.Moyo wa toba kama wa Daudi
7.Hekima kama ya selemani
8.Uvumilivu na uadilifu kama wa Ayubu
9.Upendo na Huruma kama ya Yesu

Baadaye akatoa hamasa kwa washirika kuomba Mungu akupe sifa hizo kwani kwa kuwa na hizo...waweza kuwa mkuu kuliko hao wote maana utakuwa umekusanya nyingi kuliko,moja moja walizokuwa nazo wao.

Na baadaye katika ibada ya pili Mch Matthew alifundisha juu ya UTII UNAOLETA BARAKA kwa kutumia kitabu cha Luka sura ya 5 mstari wa kwanza mpaka wa kumi na moja juu ya hadithi ya Simon na nduguze baada ya kukutana na Yesu na kutakiwa kwenda kushusha nyavu zao kilindini
1.Alisema kuna nyakati tunaona kama Yesu hajishughulishi na maisha yetu...kumbe anatutazama na ili afanye kitu kwetu anahitaji utii wetu
2.Zipo nyakati ujuzi wetu katika maisha"experinces" waweza kuwa kikwazo kwa utii wetu kwa Mungu
3.Iwe tunaamini ama hatuamini,tunatakiwa kutii hapo ndio baraka zetu zilipo.

 Matthew sasali ni Mch na Mwalimu wa Neno la Mungu,lakini pia ni meneja wa Redio Ushindi inayorusha mawimbi yake Nyanda za juu kusini,amemuoa Becky na amebarikiwa kuwa na  watoto watatu NigEl,Nicola na Natasha.

Thursday, June 28, 2012

How to Respond to False Accusition

Mara nyingi watu wamekuwa wakikosea sana kujibu...pale wanapokabiliwa na tuhuma ama wamesingiziwa huku hawakufanya jambo lile..aidha kwa hasira ama kwa kutokujua basi hujikuta unajiingiza mtegoni na kujikuta huna namna ya kutoka kisha watu huthibitisha na kusema ulihusika ama ulifanya kweli...
Pastor Matt aliona ni vizuri akushirikishe namna hii ya kujibu pale unapokabiliwa na mashitaka ya uongo...ama ni kweli hukuhusika...

1.USISEME KITU...hii hutegemea sana hali ya tukio lenyewe lilivyofikia,lakini mara nyingi mtu akikutuhumu ni vyema ukanyamaza kwanza.Waweza kuona ni kama ni ushauri wa ajabu.Ukweli ni kwamba wakati huo kiwango cha hasira huwa juu.Unajua mpaka mtu anakutuhumu yeye mwenyewe anakuwa tayari amejichanganya ama yeye tayari ana hasira.Kuna nyakati tuhuma zinatakiwa kujibiwa papo hapo...ikiwa hivyo badilisha mtazamo kwanza.Kwa upole na busara ongea na mtu ambaye amekutuhumu na kumpa nafasi ya yeye kujieleza ili kujua ukweli,hii itakusaida wewe kujipanga...tena ukiweza fanya hili mara tu.
2.TAFUTA MSAADA...tayari umeshatuhumiwa...tafuta muda na uwe makini kutafuta msaada,waweza kuwa wa kisheria,ama mashauri tu au vinginevyo.Kama huna uhakika ongea na mwanasheria azungumze nao.Usidharau hatua hii tafadhali ni muhimu sana...mambo mengine huonekana ni madogo lakini muda mfupi baadaye huwa makubwa na huchanganya akili mno...na hujikuta unapoteza uwezo wako wa kutumia akili ipasavyo.
3.KUSANYA VIELELEZO...na kwa kuwa unajua wewe huna hatia,huo ni muda wako mzuri wa kukusanya vielelezo/ushahidi ili kueleza ukweli wa jambo lako.Hivi vyaweza kuwa vya namana mbali mbali....labda ni risiti,tiketi,kumbukumbu za benki,barua pepe n.k...jitahidi kupata vielelezo vya maandishi mara nyingi huwa msaada mzuri.
4.ANDAA NAMNA YA KUJIBU...chukua vielelezo vyako na uvipangilie vizuri ili vilete mantiki kwa mtiririko unaeleweka.Mpangilio ni ufunguo mzuri wa utetezi wako.Ukituhumiwa kwa maandishi jibu kwa maandishi.
5.FANYA MAWASILIANO NA MTU ALIYE KUTUHUMU...kama una mtu wa sheria anayekusaidia tfadhali fuata maelekezo.Tafuta muda wa kukutana na mhusika kisha ongea naye kuhusu hatua unazotaka kuchukua...kuna mawili mnaweza kujikuta unamaliza wenyewe...lakini unaweza ukajikuta unakwenda ngazi ya juu zaidi.
6.FAFANUA KWA UPANDE WAKO(JITETEE)...sasa uko uso kwa uso na aliyekutuhumu...ukitoa utetezi kuhusu tuhuma juu yako...1 kumbuka kuweka hisia kali mbali...kama ulijiandaa vizuri kwa hatua za mwanzoni utakuwa na kazi rahisi tu ya kuweka ukweli hadharani 2.weka vielelezo vyako kwa mpangilio 3.wape nafasi ya kujibu....wakati huo usitarajie wakuombe msamaha...laweza kuwa hivyo ama hapana.
Wakati huo wewe utakuwa umeweka kila kitu wazi...waamuzi wanauwezo wa kuona na kuamua.
 Nahisi kwa kuzingatia ya hapo juu wewe utakuwa salama....

Sunday, June 24, 2012

Principles of Receiving from God

Pastor Matthew Sasali akiongea na wanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe,Mbeya Campus juu ya kanuni muhimu ya mtu kupokea haja yake kutoka kwa Mungu,mwishoni wa wiki hili,hii ni katika kuhitimisha semina yake ya siku tatu chuoni hapo.Pastor Matt alitaja kanuni hizo ni
1.Kuna na Uelewa wa Kutosha juu ya Mungu unayemwomba
a.Omnipresent(yuko kila mahali) b.Omniscient(anajua yote) c.Omnipotent(mwenye nguvu zote)
2.Kwa kadri unavyomwelewa Mungu,ndivyo Imani yako kwa Mungu Huongezeka
3.Ni bora kuwa na Imani ndogo kwa Mungu mkubwa,kuliko Imani kubwa kwa Mungu Mdogo.
Pastor Matt aliyasema hayo na kufanya maombi nawanafunzi hao ili kuwaandaa na mitihani yao ya kumaliza mwaka.

Friday, June 22, 2012

Udadisi ni muhimu kwa maisha ya Leo

Ulimwengu uko hivi ulivyo leo kwa sababu miaka fulani huko nyuma watu wamewahi kuwa wadadisi...ambao ulipelekea kuwa na mambo mengi mazuri na makubwa ya hivi leo.
Udadisi ni hali inayompelekea mtu kuwa "genius" mwenye ufahamu mkubwa.Sidhani kama unaweza kukuta mwna taaluma mkubwa bila nyuma yake kuwa na Tabia ya Udadisi...
Hebu tuangalie kwa nini Udadisi ni kitu cha thamani...
1....Hufanya ufahamu kujishughulisha...kutokuwa na fikra Mgando.
Watu wadadisi mara zote huuliza maswali na hutafuta tafuta majibu ya maswali hayo katika fikra zao.Ufahamu wao mara zote hujishughulisha,na kwa kadri hufahamu unavyojishughulisha ni kama misuri ya kufikiri na kupata majibu nayo hutanuka...na kwa sababu huwa tabia na zoezi la mara kwa mara...basi ule uwezo wa akili unaosababishwa na udadisi hufanyika imara na fikra hukuzwa.
2....Hufanya ufahamu wako kufungua milango ya mawazo mapya
Kumbuka pale unapoanza udadisi juu ya kitu fulani...fahamu zako huweka matarajio na kuwa tayari kupokea mawazo mapya ya jambo lile.
Na pindi wako linapokuja fahamu hulitambua na kulikubali.Bila udadisi wazo jipya laweza kukupita na kujikuta ukikosa mambo mengi kwa sababu tu ufahamu haukutayarishwa kupokea....swali kwako...mawazo mangapi mazuri,mapya yamekupita kwa sababu tu ulikosa udadisi juu ya jambo fulani?
3....hukufungulia ulimwengu mpya na yanayowezekana
Kwa kuwa mdadisi unapata fursa ya kuona ulimwengu mpya na kuvuka na kukutana na mambo ambayo ulidhani hayawezekani hapo awali...vitu vyote huwezi kuona kama si kwa udadisi.Hayo yamefichwa chini ya maisha ya kawaida (yasio ya udadisi)inahitaji udadisi kufunua na kugundua ulimwengu mwingine ambao hukuwahi kuwa kabla na kugunduka kuwa yanawezekana.

4...hufanya maisha kuwa na mvuto.
Maisha ya Udadisi ni tofauti sana na maisha ya kawaida yaliyodumaa na yanayojirudia.Maisha ya udadisi mara zote yana mambo mapya ambayo huvutia "attraction" na huwashika watu "attention".

How to Translate your dreams into the reality.

Watu wengi tunaona maisha ni magumu...lakini si kweli,ila tu hatuna ndoto za baadaye za maisha yetu.Tumesahau kuwa maisha yetu ya baadaye yanaandaliwa na heka heka za leo...wengi hatuna focus/dream/purpose ya maisha yetu...Ni muhimu kuwa na Ndoto tena si ndoto tu Ndoto kubwa.
Na wengine wamekuwa na Ndoto nyingi tena nzuri...Tatizo linakuja namna ya kuifanya ndoto hiyo iwe halisia "reality"
Mch Matthew Sasali aliyasema hayo kwa wanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe tawi la Mbeya katika semina iliyoanza jana katika kuwaweka vizuri kwa habari ya maandalizi yao ya mitihani ya mwisho inayotarajiwa kuanza juma lijalo.
Pastor Matthew,aliweka hamasa kubwa ya kuwa na Ndoto ya maisha yao ya baadaye akitumia Mfano wa Yusufu katika kitabu cha mwanzo 37...ambaye aliona maisha yake miaka mingi ijayo.
Akiendelea kufundisha alisema yako mambo muhimu ambayo kila mwenye ndoto anatakiwa kuishi...ni kama mama mjamzito siku anapojigundua ana kitu tumboni mwake...kila kitu hubadilika na mfumo mzima wa maisha hubadilia ili kuhakikisha ndoto ya mtoto kuzaliwa inatimia.
Pastor akafundisha Vitu Kumi...kwa kupitia Neno "DEDICATION" herufi moja kwenda nyingine
Depend on Holy Spirit,Endure Hardships,Define your Focus,Internalization,Courage,Attitude(Descipline),Take Risk,Inspiration,Open your Mind(Exposure), na Never Give up.
Na mwisho kabisa Mch Matthew alipata fursa ya kuomba pamoja nao...Bwana awape Ndoto na kwa wengine...kutembea katika hayo...na kwa wote kwa ajili ya maandalizi ya mitihani yao.
Pastor Matthew ni Mchungaji,pia ni Meneja wa kituo cha Redio Ushindi Mbeya na sehemu kubwa ya huduma yake ni kwa wanafunzi wa vyuo.

Monday, June 11, 2012

What we Miss is Commitment

Siku ya jumapili ya tarehe 10/06/2012 Pastor matthew Sasali alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Graduation ya wanafunzi wa Chuo kikuu Mzumbe(USCF-Mbeya Campus)na kupata nafasi ya kutoa changamoto kuhusu mambo ya kiroho,maisha ya kila siku na kisiasa pia.
Sherehe hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya,Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Mkuu wa chuo hicho Campus ya Mbeya...ambaye aliwaasa wanafunzi kufanya bidii,kujituma huku wakiepuka vishawishi ambavyo vinaweza kuwaharibia maisha yako na kupata magonjwa kama ukimwi.
Pastor Matt alieleza kuwa Taifa letu lina wasomi wengi,wataalam wa kila aina,rasirimali nyingi...ila limekosa watu walio COmmitted kwa ajili ya kuinua Taifa letu...aliendelea na kusema Commitment hujengwa tangu ndogo mpaka Kubwa hutokea...na kwa kizazi hiki huu ndio wakati wa kuanza kujenga Commitment...hivyo hupelekea mafanikio katika weledi wao pindi wanapoingia kazini.
 Pastor Matthew Alipata tena wasaa wa kuongea na wanafunzi hao juu ya siasa ya nchi yetu...na kuanza kujenga ushawishi wa kuwataka vijana hao wawe wa kwanza kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali kwani kilio kikubwa cha taifa letu ni kukosa viongozi waadilifu...Lakini kwa wao kugombea nafasi mbali mbali na kisha kupata nafasi hizo zinaleta mabadiliko,ustawi na uponyaji wa kwa Taifa letu kwa kuwa wao wana kitu cha Ziada nacho ni UCHAJI WA MUNGU.

Careful with Opportunities

Leo yamkini tusingekuwa hivi tulivyo kama tungetumia fursa fulani zilizowahi kujitokeza kwenye maisha yetu...yamkini tumebaki na majuto lakini hakuna namna ya kuziba.
Mara zote ukipoteza fursa fulani kwenye maisha huwezi kukwepa kuijutia.
Hayo yalisemwa na Pastor Matthew Sasali alipokuwa akiongea na wanachuo wa chuo cha MMTC Mbeya Medical Training Center kilichopo Hospital ya Rufaa Mkoani Mbeya,wakati wa sherehe za Graduation kwenye fellowship ya wapendwa chini ya mwamvuli wa TAFES.
Aliongeza na kusema,mara nyingi watu wamekuwa na kawaida ya kudharau mambo yanayowatokea huku wakidhani yatatokea tena...hivyo hawako makini hata kwa fursa ambazo kumbe hazirudii tena.
Kwa kuelezea akatoa mfano na kusema kama tungerudishwa nyuma na kuwa sekondari hivi tulivyo sasa,wengi wakasema tungefanya vizuri zaidi ya tulivyofanya wakati ule...sababu:wengi hawakujua kuwa muda ule na madarasa yale ni fursa ambayo ilitakiwa itumiwe vizuri na kujenga future nzuri baadaye.
 Mkazo mkubwa ilikuwa ni kuwa makini kwa Neno la Mungu ambalo huja kama nafasi adimu ili kutuinua...kuwa makini kwa watu ambao Mungu huwaleta kwenye maisha yetu...,matukio mbali mbali ambayo yamkini huwa kama ngekewa na hayarudii tena....Maana humo ndio kuliko na nafasi zetu za kutoka na kuchanua.Na mwisho kulikuwa na chakula cha Pamoja katika kufurahia miisho hiyo ya kuagana.
Mchungaji Matthew Sasali pia ni meneja wa Redio Ushindi Mbeya amekuwa na huduma kubwa kwa  wanafunzi wa vyuo akifundisha neno la Mungu na kujenga ushawishi na pia kuleta changamoto namna wanavyofikiri.