Monday, June 11, 2012

Careful with Opportunities

Leo yamkini tusingekuwa hivi tulivyo kama tungetumia fursa fulani zilizowahi kujitokeza kwenye maisha yetu...yamkini tumebaki na majuto lakini hakuna namna ya kuziba.
Mara zote ukipoteza fursa fulani kwenye maisha huwezi kukwepa kuijutia.
Hayo yalisemwa na Pastor Matthew Sasali alipokuwa akiongea na wanachuo wa chuo cha MMTC Mbeya Medical Training Center kilichopo Hospital ya Rufaa Mkoani Mbeya,wakati wa sherehe za Graduation kwenye fellowship ya wapendwa chini ya mwamvuli wa TAFES.
Aliongeza na kusema,mara nyingi watu wamekuwa na kawaida ya kudharau mambo yanayowatokea huku wakidhani yatatokea tena...hivyo hawako makini hata kwa fursa ambazo kumbe hazirudii tena.
Kwa kuelezea akatoa mfano na kusema kama tungerudishwa nyuma na kuwa sekondari hivi tulivyo sasa,wengi wakasema tungefanya vizuri zaidi ya tulivyofanya wakati ule...sababu:wengi hawakujua kuwa muda ule na madarasa yale ni fursa ambayo ilitakiwa itumiwe vizuri na kujenga future nzuri baadaye.
 Mkazo mkubwa ilikuwa ni kuwa makini kwa Neno la Mungu ambalo huja kama nafasi adimu ili kutuinua...kuwa makini kwa watu ambao Mungu huwaleta kwenye maisha yetu...,matukio mbali mbali ambayo yamkini huwa kama ngekewa na hayarudii tena....Maana humo ndio kuliko na nafasi zetu za kutoka na kuchanua.Na mwisho kulikuwa na chakula cha Pamoja katika kufurahia miisho hiyo ya kuagana.
Mchungaji Matthew Sasali pia ni meneja wa Redio Ushindi Mbeya amekuwa na huduma kubwa kwa  wanafunzi wa vyuo akifundisha neno la Mungu na kujenga ushawishi na pia kuleta changamoto namna wanavyofikiri.

No comments:

Post a Comment