Thursday, August 23, 2012

Dr Mtokambali askofu tena TAG

Ilikuwa na Nderemo na vifijo katika ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma,baada ya msimamizi wa Uchaguzi mwenyekiti wa wameshinari Africa Mashariki Rev.Gregory Beggs,kutangaza kuwa Dr Barnabas Wenston Mtokambali,ameshinda uchaguzi kwa Kura zaidi ya 1900 sawa na asilimia 93 ya wapiga kura wote.
Haikuwa rahisi kuamini hilo kwa Askofu Mtokambali,hivyo kumfanya atokwe na Machozi na kisha kuanza kuwashukuru Wajumbe wa mkutano huo na kutoa Ahadi ya kukubali uteuzi huo na kuwa yuko tayari kulitumikia shauri la Mungu kwa kipindi kingine tena cha miaka minne.
 Kabla ya Uchaguzi huo,Askofu mtokambali alitangulia kusoma ripoti ya utendaji kazi kwa kipindi chake cha kwanza cha miaka minne iliyopita,ambayo ilisheheni mambo makubwa ambayo yeye na kamati yake wamefanikiwa kuyatekeleza na kuyaanzisha,chini ya sera maarufu ijulikanayo kama MIAKA KUMI YA MAVUNO,ripoti hiyo ilionyesha namna gani gani kanisa lilivyoongezeka maradufu kimapato,kimaendeleo,kihuduma,kiidadi,watumishi na hata kimahusiano na serikali na hata kimtandao nje ya nchi.Ripoti ambayo ilichukua takribani saa moja na nusu kusomwa kwa wajumbe na kisha kushangiliwa kwa nguvu na maombi mengi ya shukrani kwa kile Bwana alichokuwa anakifanya na kanisa la TAG.
 Na punde tu baada ya kumaliza ripoti yake,Askofu atokambali alitumia dakika takribani kukemea vikali kampeni vilizokuwa zikiendelea chini kwa chini kuhusu uchaguzi huo,na kusema si sera wala mlengo wa kanisa hilo kufanya kampeni katika mchakato wake wa uchaguzi nyanja zote,na kama kanisa limefika huko liko hatarini kuachwa na Mungu.
Maneno hayo aliyasema baada ya kuwa na vuguvugu la kampeni za kikabila,kuchafuana,kielimu na hata kifedha zilizojipenyeza katika harakati za kuelekea mkutano huo wa Uchaguzi.
Dr Mtokambali alifanikiwa kuchaguliwa tena kuwa askofu mkuu wa kanisa hilo kwa miaka minne mingine kwa Mujibu wa katiba ya kanisa la TAG.
Hata hivyo,Dr magnus Mhiche aliyekuwa makamu askofu Mkuu naye alifanukiwa kurudishwa tena katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minne mingine,na kisha uchaguzi wa ngazi ya kitaifa ulikamilika baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa kanisa hilo Rev.Ron Swai maarufu kama "Chalii"kurudishwa tena katika nafasi hiyo vile vile kwa miaka minne mingine.
 Mkutano huo wa Uchaguzi kwa mijibu wa katiba ya TAG hufanyika kila baada ya miaka minne,na kamati hii iliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2008 na kuja na sera ya MIAKA KUMI YA MAVUNO ambayo imeleta dira ya maendeleo ya kanisa hilo kwa kiasi kikubwa.
Dr Barnabas W.Mtokambali,alizaliwa miaka takribani 50 iliyopita,wilayani Chunya,wazazi wake wakiwa ni wahamiaji kutoka maeneo ya ziwa Nyasa(Manda),alianza safari yake ya masomo Mkoani Kigoma(form 1&2)kisha kuhamia Sekondari ya Forest(Mkoani Morogoro) na kisha Alipata Elimu ya Juu(BA)East African School of Thelogy nchini Kenya na baadaye M.Div,M Th na kisha D.Min vyuo mbali mbali nchini Marekani kati ya miaka ya 1992 na 2005.
Alianza huduma miaka ya 1988 mjini morogoro kanisa na Bethel Revival Temple ambalo analichunga Mpka sasa kutoka utupu mpaka takribani washirika 2000 hivi sasa.
Amemuoa Mrembo GLADMERRY maarufu kwa jina la MAUA na amebarikiwa watoto watatu,JOYLINE(chuo kikuu)GLADYLINE(High school) na wa kiume Pekee OCEANNIC(primary school).
Dr Mtokambali ana historia ndefu kwa kanisa hili na katika uongozi wa kanisa hili tangu mwaka 1992 mpaka sasa amewahi kuwa Katibu wa sehemu ya Morogoro,makamu askofu wa jimbo la Mashariki,Askofu nwa jimbo la Morogoro,makamu askofu Mkuu na sasa ni askofu Mkuu.
Ni mhadhiri wa vyuo vikuu duniani(global University),Mwalimu wa Neno la Mungu,Mbeba maono ya vyuo vya kupanda makanisa na mtandao wa ujenzi wa makanisa Africa,Mchungaji wa kanisa na mahali pamoja,Mume na Baba wa Familia na mambo mengine mengi.
 Huyu Ndiye Askofu wa kanisa la TAG Dr barnabas Mtokambali.

No comments:

Post a Comment