Monday, July 30, 2012

Mkristo na Ulimwengu unaobadilika

"Namshukuru Mungu kwa nafasi hii ya kipekee sana ya mimi kuhudumu ndani ya kanisa la kilutheri tangu nimeanza kumtumikia Mungu na kanisa langu la TAG...." hayo ni baadhi ya maneno yaliyosemwa na Pastor Matthew Sasali alipokuwa akijitambulisha katika kanisa la Lutheran Forest jijini Mbeya.
Pastor Matt amekuwa na juma moja la kuhudumu na kanisa la Lutheran,Usharika wa Forest tangu tarehe 23/07 hai tarehe29/07...na hii na katika maadhimisho ya wiki la sikukuu ya vijana kanisani hapo,ambayo shamrashamra zake zilianzia jumatatu hiyo kwa semina ya vijana wote hapo kanisani kisha kilele chake kilikuwa siku ya jumapili kwa Pastor Sasali kuhudumu katika idaba zote mbili za kanisa hilo na kisha katika idaba ya jioni ya kusifu na kuabudu iliyokuwa ikiongozwa na Praise and Worship Team kutoka Kanisa la Agape(Redeemed)inayojulikana mjini Mbeya kama Super Power chini ya Mwalimu na Producer Fredy Kametta.
 Kichwa cha Ujumbe wa semina hiyo ilikuwa ni Kijana mkrist na ulimwengu unaobadilika;ambapo Pastor Matthew alifundisha kuhusu Mtazamo wa Mungu juu ya Vijana,na kusema Mungu ameweka Hazina kubwa ndani ya vijana na Mungu amewaamini vijana kwa kuwa wana nguvu,Maono na wamemshinda shetani.
Pia alisema juu ya Mtazamo wa Kanisa kwa Vijana;alieleza namana ambayo kanisa la leo halimwamini kijana na kumuona ndiye chanzo cha machafuko na vurugu ndani ya kanisa.Na aligusia kuhusu Mtazamo wa Ulimwengu na Shetani kwa vijana,ambapo kijana hutumika kama chombo cha uharibifu dhidi ya ufalme wa Mungu.
 Pastor Matt akiendelea kufundisha alionyesha kielelezo cha vijana wa biblia ambao maisha yao yamekuwa chachu kwa vijana wa kikristo kama vile Yusufu,Daniel na wenzake,Daudi n.k
Haikuwa rahisi kwa Mchungaji Matthew kuhudumu ndani ya kanisa la kilutheri,maana ni kanisa lenye taratibu tofauti na kanisa asili la Mch Matthew,lakini kwa kuwa wote hulitaja jina la Bwana na kujenga ufalme wa Mungu...haikuwa shida kwake kuhudumia Neno la Mungu kanisani hapo,na kufuata taratibu zote za kikanisa.
Na jioni katika ibada ya kusifu na kuabudu Pastor Matthew alisema imekuwa rahisi sana kwa watu kuwasifia wapenzi wao,kutumia muda mwing na wapenzi wao na kujitoa kwa kiwango cha juu kwao hivyo hupelekea kuboresha mahusiano yao na wanao wapenda...lakini imekuwa kunyume kwa Mungu,wakristo hawana maneno mengi na mazito ya kusifu na kumwabudu Mungu wala Muda wa kutosha na Mungu hivyo kufanya mahusiano yao na Mungu kudhoofu kila iitwapo leo...alihamasisha na kusema Uimbaji ni njia rahisi ya kufunua hisia za mtu,hivyo katika ibada hivyo  ya kusifu na kuabudu tuitumie kama ni nafasi adimu katika maisha yetu ya kueleza hisia zetu kwa Mungu.

1 comment:

  1. utandawazi ukitumiwa vizuri unaweza kuwa chachu ya vijana wengi kumjua Mugu na mapenzi yake kwetu.by Baraka zakayo mungure

    ReplyDelete