Tuesday, September 18, 2012

Dr Mwanjoka asimikwa

Baada ya Uchaguzi wa August 9,pale UDOM wa kanisa la TAG,jimbo la Nyanda za Juu Mbeya lilipata askofu Mpya Dr Donald Mwanjoka ambaye leo amesimikwa na hivyo kutangazwa rasmi kuwa ndiye askofu wa Nyanda za juu Mbeya.
Ibada hiyo ya kusimikwa iliongozwa na askofu Mkuu wa kanisa la TAG,Dr Barnabas Mtokambali.
Kabla ya kuanza tendo hilo la kuwasimika,Askofu Mtokambali aliweka wazi utaratibu wa kuwapata viongozi wa kanisa la TAG na alisema wanapatikana kwa njia ya Maombi na si kwa Kufanya kampeni,kwa ubaguzi wa kikabila ama kwa kutoa rushwa...hivyo akamalizia na kusema Dr mwanjoka ndiye Chaguo la Mungu kwa wakati huu baada ya Mungu kujibu maombi ya waamini,washirika na kanisa kwa ujumla.
Pia Dr Mtokambali alitumia nafasi hiyo kufikisha ujumbe kwa serikali...na alisema serikali yetu inatakiwa kutumia nguvu zake zote katika kulinda Amani ya Nchi yetu,Ushirikiano na Umoja wetu.
Pamoja na Dr Mwanjoka,walisimikwa pia makamu askofu wa jimbo Rev Adson Mwajunga na katibu Rev.Peter Masika.
 Sherehe hizo zilifanyika katika kanisa la ICC-Ikuti(International Christians Centre) ambalo ni kanisa linalochungwa na Askofu Dr Donald Mwanjoka.Leo tarehe 18/09/2012 kuanzia saa 3 asubuhi mpaka na kumalizika majira ya saa 10 jioni
Pamoja na hayo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya ambaye hata hivyo hakuweza kufika aliwakiliswa na DAS(katibu Tawala).

No comments:

Post a Comment