Sunday, August 26, 2012

Steps to becoming the Vessel of Honour

Ili kuwa mtu wa kiMungu ambaye watu wata-admire maisha yako,lazima upite kwenye mchakato waKiMungu(God`s person thru God`s process),Na mara zote mchakato wa kiMungu si mwepesi.
Mara zote Mungu hufanya kazi kuhakikisha,tunakaa katika ile taswira ambayo ameikusudia katika maisha:hayo yalisemwa na Pastor Matthew sasali katika utangulizi wa ujumbe wake asubuhi ya leo,katika kanisa la Rehoboth International Christian Centre,jijini Mbeya wakati wa mahubiri yake,ibada ya kwanza na ya pili.
  Kifungu kilichotumika ni Yeremia 18:1-6,wakati Mungu akimsikilizisha Nabii Yeremia neno lake juu ya Taifa la Israel.
Pastor Matthew alisema,kama unataka kuwa chombo cha heshima kwa ajili ya huduma ya kiMungu,ni lazima ukubali kuchongwa na Mungu kwa namna ile ambayo Mugnu mwenyewe anataka...na hiyo ni kazi ya MUNGU mwenyewe.
Kabla ya kuanza kutaja hatua hizo alitaka kanisa lijue mambo mawili kwanza ya msingi
1.Taswira ya chombo kinavyotakiwa kuwa iko mawazoni mwa Mfinyanzi mwenyewe
Watu wengi hudhani wao ndio wanaoweza kutabiri na kufanya kile ambacho wao hutamani katika huduma zao...mwisho wa siku tunatengeneza matakwa yetu na si matakwa ya Mungu.
2.Sisi kama udongo na Mungu kama mfinyanzi ni lazima kwa unyenyekevu na adabu,tukubali kukaa mikononi mwa mfinyanzi ili mwisho wa Mchakato tuwe kile ambacho Mungu amekusudia.
Ni rahisi kukosa unyenyekevu na subira na kukimbia katikati ya mchakato,na wengi hufanya hivyo...mwisho wa siku,hatutokei kile ambacho mfinyanzi amekikusudia.
Akaendelea na kusema Mungu yeye kama mfinyanzi anayajua maisha yetu ya zamani,ya sasa na ya baadaye,hivyo wakati anafanya kazi yake na sisi tayari anakuwa ameona kile ambacho tunatakiwa kukikamilisha katika maisha yetu ya baadaye.
 Hatua za Kuwa chombo cha Heshima
1.Ni lazima mfinyanzi akusanye Udongo kutoka ardhini na kisha autenge na uchafu(ausafishe).
Ili kuwa chombo cha heshima,lazima ukubali kutakaswa na kuoshwa dhambi kwanza,maana huwezi kufika ngazi ya kuwa chombo cha Heshima huku ukiwa mwenye dhambi,la sivyo chombo kilichotengezwa bila udongo wake kuoshwa ipasavyo ni rahisi kuvunjika hata kama kinang`aa namna gani.
2.Mchakato huo wa Kuoshwa kwa udongo hukamilishwa na Maji...udongo hulowekwa ili kuuchambua na kisha kuwa laini ili kumrahisishia mfinyanzi kufanya atakavyo...maji ni Roho mtakatifu,Mtu wa Mungu lazima awe na ujuzi binafsi na roho mtakatifu maana humo ndimo karama,huduma,tabia,mienendo hulainishwa na kufanywa utayari kwa mfinyanzi kumtumia mtu.
3.Ukitazama picha ya Mfinyanzi,utadhani anazombana na udongo katika hatua hii ila kufanya chombo,na hii ndio hatua ambayo chombo huumbika.
Si hatua rahisi na laini,watu wengi hukimbia hatua hii...hapa ni wakati unafinyangwa,ni wakati wamaumivu,kukataliwa,kukosa chakula ama mavazi,kuachwa na marafiki...nyakati ngumu hata kutengwa ndani ya kanisa...si hatua rahisi,maana Mungu anashughulika mna maisha yako ili kufikia kusudi lake,anashughulika na tabia yako ili kukufanya ufae..wengi hukimbia hatua hii ya mchakato wa kiMungu...maana huona ni kama Mungu amemwacha na kama hujagundua kuwa uko kwenye mchakato wa kiMungu,huwa tunatumia muda mwingi kufunga na kuomba na kukemea ili hali hii ipite kando...kumbe Mungu hutucheka na kusema"huyu ni yeye mwenyewe aliomba kufinyangwa ili afae...mbona anataka kukimbia tena..."mara zote yeye anatuwazia yaliyo mema.
Kuna nyakati tunapitia kwenye nidhamu na kuona kama tunaonewa...kumbe Mungu anatuwazia yaliyo mema kwa maisha yetu ya utumisha wa baadaye.
Tukitoka kwenye hatua hizo...kila mtu hutamani huduma yetu,maisha yetu,baraka zetu,mafanikio yetu....lakini tukumbuke ili tuwe mtu wa kimungu kama alivyotukusudia ni lazima tupite kwenye mchakato wa kiMungu.

Akamaliza na kusema tunatamani maisha ya Yusufu,Ayubu,Musa,Daudi na wengine wengi kwenye biblia...siri kubwa ni lazima tuwe na unyenyekevu na kukubali kubaki kwenye mikono ya mfinyanzi hata nyakati za kufinyangwa kwetu.

No comments:

Post a Comment