Sunday, May 20, 2012

Your response is Your Breakthruough

Watu wengi wamekuwa wakitafuta Mpenyo katika maisha yao huku wakisahau kanuni muhimu ya ki-Mungu ili kupata mpenyo huo.
hayo yalisema na Rev Matthew Sasali katika kanisa la Yerusalem Temple jijini mbeya alipokuwa akihudumu jumapili hii.
Mchungaji Matthew ambaye pia ni Meneja ya Redio Ushindi jijini Mbeya aliongeza na kutaja kanuni muhimu za kuzifata ili watu waweze kuona mpenyo katika maisha yao...nazo ni :
1.lazima uitikie kwa namna chanya juu ya Neno la Mungu
2.Lazima uitikie chanya kwa fursa zinajitokeza katika maisha ya kila siku
3.lazima utikie chanya kwa watu wanaokuzunguka katika maisha yako
4.Lazima uitikie chanya kwa matukio hasa ya kijamii

Mchungaji Matthew alimaliza kwa kuwataka wakristo kuwa makini katika maisha yao ya kila siku kwani hakuna ajuaye ni wapi hasa mpenyo wa maisha yake utatokea.
Na baadaye jioni Mch.Matthew Sasali aliwabatiza waumini wapya wa kanisa.

No comments:

Post a Comment